Simba kupunguza wachezaji ‘mizigo’

No Comments

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zakaria Hans Poppe amesema baada ya kushindwa kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa, wanaangalia mbele na kujipanga upya kwa msimu ujao.
Awali, moja ya malengo makubwa waliyojiwekea klabu hiyo ni kuchukua taji la ligi, lakini mambo yalikuwa tofauti kwao, wakizidiwa kete na watani wao wa jadi, Yanga.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, alisema wataangalia namna ya kuwapunguza wachezaji mizigo, na kusajili nyota watakaokuwa na msaada kwa timu ili msimu ujao ije kivingine.
Mwenyekiti huyo alisema huenda wakaachana na baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao walikuwa na mgomo baridi hivi karibuni na hata kugomea safari ya Songea kuumana na Majimaji katika mchezo wa Ligi Kuu, ikidaiwa walikuwa wanashinikiza kulipwa mishahara yao.
Hata hivyo, alisema hatima yao itategemea na maamuzi ya kikao chao cha kamati ya utendaji kitakachoketi siku za hivi karibuni.
Simba iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mara 18 ikizidiwa na Yanga iliyotwaa mara 26, ilipania ubingwa msimu huu, lakini ikajikuta inapoteza mwelekeo katika hatua za mwisho za ligi, hasa baada ya kudundwa 1-0 na Mwadui FC ya Shinyanga.
Mpaka sasa, Simba iliyotwaa ubingwa wa Bara mara ya mwisho katika msimu wa 2011/2012 iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 29 na imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani. Azam ni ya pili, ikiwa na pointi 6
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment