Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zakaria Hans Poppe amesema baada ya kushindwa kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa, wanaangalia mbele na kujipanga upya kwa msimu ujao.
Awali, moja ya malengo makubwa waliyojiwekea klabu hiyo ni kuchukua taji la ligi, lakini mambo yalikuwa tofauti kwao, wakizidiwa kete na watani wao wa jadi, Yanga.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, alisema wataangalia namna ya kuwapunguza wachezaji mizigo, na kusajili nyota watakaokuwa na msaada kwa timu ili msimu ujao ije kivingine.
Mwenyekiti huyo alisema huenda wakaachana na baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao walikuwa na mgomo baridi hivi karibuni na hata kugomea safari ya Songea kuumana na Majimaji katika mchezo wa Ligi Kuu, ikidaiwa walikuwa wanashinikiza kulipwa mishahara yao.
Hata hivyo, alisema hatima yao itategemea na maamuzi ya kikao chao cha kamati ya utendaji kitakachoketi siku za hivi karibuni.
Simba iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mara 18 ikizidiwa na Yanga iliyotwaa mara 26, ilipania ubingwa msimu huu, lakini ikajikuta inapoteza mwelekeo katika hatua za mwisho za ligi, hasa baada ya kudundwa 1-0 na Mwadui FC ya Shinyanga.
Mpaka sasa, Simba iliyotwaa ubingwa wa Bara mara ya mwisho katika msimu wa 2011/2012 iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 29 na imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani. Azam ni ya pili, ikiwa na pointi 6

Simba kupunguza wachezaji ‘mizigo’

admin
,
Na Selemani Abeid, Shinyanga WAMEKAA! Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, hatimaye Simba wamefanikiwa kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya jana kuichapa Stand United kwa bao 2-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. Bao la Simba lililowafanya wakae kileleni liliwekwa kimiani na Hamis Kiiza dakika ya 34, baada ya kupata pande safi kutoka kwa Ramadhan Kessy. Hii ilitokana na Simba kugongeana pasi safi, kabla ya kumkuta Kessy aliyemimina krosi maridadi kwa Kiiza aliyemchungulia golikipa Frank Muwonge na kumtungua. Dakika ya 51, Kiiza kwa mara nyingine aliifungia Simba bao la pili kutokana na juhudi zake binafsi. Hilo linakuwa bao la 16 kwa Kiiza, ambaye sasa ndiye anayeongoza kwa mabao akifuatiwa na Amisi Tambwe wa Yanga aliye na mabao 14. Ushindi huo, umeifanya pia Simba ikae kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 45, wakifuatiwa na Yanga walio na pointi 43, huku Azam ikiwa na pointi 44. Azam wanaweza kusogea nafasi ya pili kama watashinda katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mchezo huo ulikuwa na kosakosa kadhaa, lakini nafasi ambazo Simba watazijutia ni ile ya dakika ya 49, pale Ibrahim Hajib aliposhindwa kufunga akiwa amebaki na lango. Kiiza pia alipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 37, baada ya kupewa pasi safi na Said Ndemla na kushindwa kulenga lango. Stand United: Frank Muwonge, Revocatus Richard, Seleman Mrisho, Nassor Masoud, David Osman, Jacob Massawe, Pastory Athanas, Amri Kiemba, Elius Maguli, Seleman Salembe, Vitalis Mayanga. Simba: Vicent Angaban, Hassan Kessy, Emery Nimubona, Abdi Banda, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamis Kiiza, Ibrahim Ajib, Said Ndemla.

Simba yakaa kileleni

admin
,
Previous PostOlder Posts Home